MANONGA CLASSIC AANIKA HISTORIA YA MAISHA YAKE,ALIWAHI KUWA MVUMVI NA KUNUSURIKA KULIWA NA MAMBA

 
Mwimbaji wa nyimbo za injili anayeitwa Manonga Classic hivi karibuni kupitia mtandao wa facebook ameelezea historia ya maisha yake,aliyoipatia jina la 'Mkasa wa Mama wa kambo'.

Katika historia hiyo Manonga anaeleza ushuhuda wa maisha yake na changamoto mbalimbali alizozipitia maishani na jinsi ambavyo Mama yake wa kambo alivyompitisha katika magumu.Ushuhuda huo una sehemu tano hivyo karibu sasa uweze kupitia sehemu moja baada ya nyingine upate kufahamu kuhusu mkasa wote.



PAUL MICHAEL MANONGA NDIO JINA LANGU HALISI...MANONGA CLASSIC NI JINA LA KAZI ZANGU KWA MAMA YANGU MZAZI MIMI NDIO MTOTO WA KWANZA NA WA MWISHO MWANAUME.NIMOJA KATI YA MTOTO NILIEPITIA MAISHA YA KUISHI NA MAMA WA KAMBO TAKRIBANI MIAKA SITA ILIYOPITA HUKO NYUMA.

MAPENZI KWA BABA YANGU YALIKUWA NIMAKUBWA SANA ALINIPATIA MAHITAJI YOTE NA MAPENZI YOTE KAMA MTOTO WAKE PESA NZURI YA MATUMIZI YA SHULE ALINIPA NILIISHI KWA FURAHA NA AMANI NIKIWA NAUFURAHIA UPENDO WA BABA JUU YANGU.

BAADA YA MAMA WA KAMBO KUONA MAPENZI YA BABA YAMEZIDI KWETU MAMA WA KAMBO ALIANZA KUPATA USHAURI KUTOKA KWA MARAFIKI ZAKE MBALIMBALI JINSI YA KUUPUNGUZA UPENDO KWA BABA JUU YETU. SIKU MOJA BABA AKIWA AMEONDOKA KWENDA KAZINI NDIPO NA MAMA WA KAMBO ALIPOTOKA PASIPO KUTUAGA AMA KUJUA AMEKWENDA WAPI.

ALIPORUDI ALIRUDI NA CHUPA NDOGO IKIWA INAJUICE YA RANGI NYEUSI AMBAYO NDANI YAKE ILIKUWA INAMADUDE MEUSI AMBAYO YALIKUWA NIMADAWA ALIYOPEWA NA MGANGA WAKE ATUCHANGANYIE NDANI YA JUICE ILI TUKINYWA TUWEZE KUPUMBAZIKA AKILI AMA TUWE MACHIZI KABISA.NDIPO ALIPOMKUTA MDOGO WANGU NA KUMUONYESHA UPENDO WA HALI YA JUU AMBAO HAIKUWAHI KUTOKEA SIKU ZOTE.

NDIPO AKAMPA ILE JUICE ANYWE ILA KWA MASHARTI MOJA ATUMIE KIKOMBE CHEKUNDU MBILI AHAKIKISHE NA MIMI NIMEKUNYWA MDOGO WANGU ALIPOTAKA KUTUMIA KIKOMBE KINGINE ALIZUILIWA NA ALIPOTAKA KUMPA MTOTO WAKE MDOGO AMBAE NIWAMAMA WAKAMBO AKIWA ANATEMBEA AKAMWAMBIA WATOTO WADOGO HUWA HAWANYWI JUICE.

NDIPO MDOGO WANGU ALIPOSHITUKA KWA NINI ANIAMBIE NITUMIE KIKOMBE CHEKUNDU WAKATI MDOGO WANGU AKIWA ANAKUNYWA JUICE ILE NDIPO AKASIKIA KAMA MKONO UNAKUWA MZITO SANA KUIPELEKA MDOMONI JUICE ILE NA NAFSI INAMWAMBIA USINYWE LAKINI PASIPOKUJUA MDOGO WANGU ALIKUNYWA NAMI AKANILETEA
NILIPOIFUNGUA KITENDO CHA KUPELEKA TU MDOMONI MKONO WANGU UKAWA NIMZITO KABISA NIKAMUULIZA MDOGO WANGU MBONA MKONO UNAKUWA MZITO KUNYWA HII JUICE AKANIAMBIA HATA MIMI NILISIKIA MKONO MZITO KABISA NA CHAAJABU ALINIAMBIA NITUMIE KIKOMBE CHEKUNDU.

NILIINYWA JUICE ILE KIDOGO BAADAE RAFIKI YANGU KIPENZI ALINIOMBA NAE ANYWE SIKUWEZA KUMNYIMA KWA SABABU SIKUJUA KILICHOKUWA KINAENDELEA NA HAIKUWAHI KUTOKEA NIKAMNYIMA KITU.

MATARAJIO YA YULE MAMA BAADA YA KUINYWA JUICE ILE ALISUBIRIA KUONA MATOKEO YATAKAYOKUJA KUTOKEA
ASHUKURIWE MUNGU ATUEPUSHAE NAMAMBO TUSIOWEZA KUYAONA KWA MACHO YA KIBINADAMU NA ASHUKURIWE PIA YEYE ALINIJUA TANGU NIKIWA TUMBONI MWA MAMA YANGU YAKUWA SIKU MOJA NITAKUWA MTUMISHI WAKE.

NILIPORUDI NYUMBANI MAMA WA KAMBO ALINICHANGAMKIA SANA NA AKANIULIZA VIPI MDOGO WAKO ALIKULETEA ZAWADI NIKAMJIBU NDIO AHSANTE AKANIULIZA TENA BAADA YA KUNYWA UMEJISIKIAJE NIKAMJIBU NIKO SALAMA KABISA NA NIKO SAWA TU.

BADO NIKO KWENYE MKASA WA MAMA WA KAMBO
...Itaendeleaaaaa...Usikose sehemu ya pili.  
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment