MUHUBIRI ALIYETABIRI KIFO CHA RAISI MUGABE BADO YUPO MATATANI KESI YAKE KUENDELEA
Jaji mkuu Luke Malaba amesema kuwa njia iliochukuliwa kuwasilishwa kwa kesi hiyo mbele ya mahakama ya kikatiba ina dosari.
Kesi hiyo haitarudishwa katika mahakama ya hakimu ,ambapo muhubiri Mugadza , kiongozi wa kanisa la Remnant ameshtakiwa kufanya uhalifu.
Alijipata mashakani baada ya kutabiri mnamo mwezi Januari kwamba rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 atafariki tarehe 17 mwezi Oktoba.
Wakati alipokamatwa, wakili wake Gift Mtisi aliambia BBC: Amekiri ukweli. Anasema hakudanganya -huo ni ujumbe kutoka kwa mungu.
Polisi watalazimika kuthibitisha kuwa Mungu hakuema.
Wakili wa muhubiri wa Mugadza aliitaka mahakama ya kikatiba kufutilia mbali mashtaka hayo kwa kuwa yanakiuka uhuru wake wa kujieleza.
Upande wa mashtaka unasema kuwa muhubiri huyo aliitusi dini ya Kikristo na utamaduni wa Kiafrika kwa kutabiri kifo cha Mugabe.
Kutabiri kifo cha kiongozi ni makosi kulingana na imani za kitamaduni.
Source:BBC
0 maoni:
Post a Comment