SEHEMU YA TATU YA MKASA WA MAMA WA KAMBO-JINSI NILIVYONUSURIKA KULIWA NA MAMBA
Karibu uendelee na simulizi ya Ushuhuda wa kweli wa Mwimbaji wa nyimbo za injili anayeitwa Manonga Classic inayoitwa 'Mkasa wa mama wa kambo',leo tupo katika sehemu ya 3.
BAADA YA KUWA TUMEPATA TAARIFA YA KIFO CHA BABA YANGU MZAZI NA ALIYEKUWA WA KWANZA KUNIPA TAARIFA HIZI ALIKUWA NIMAMA YANGU MZAZI.HUZUNI UCHUNGU MKUBWA NA MAJONZI NA HUZUNI NYINGI VILIIKUMBA FAMILIA YETU NILIUMIA KUMPOTEZA BABA YANGU NA IKUMBUKWE ALIPOTEZA MAISHA AKIWA NA CHUKI NA MIMI ILIYOSABABISHWA NA MTU TU.
TARATIBU ZA KUANZA SAFARI KWENDA KUMZIKA BABA YANGU ZILIANZA HATIMAE TUKAFANIKIWA KUFIKA MSIBANI NA NDIPO NILIPOKUTA BABA YANGU AMEKWISHA FUKIWA PASIPO SISI WATOTO WAKE KUMUONA MAUMIVU HAYAKUKOMA KWANGU SABABU NILIPOTEZA MTU MUHIMU AMBAE HATA SAUTI YA MWISHO NA MANENO YENYE HEKMA NA BUSARA KWAKE SIKUYAPATA.
SIMU YA BABA YANGU ALIYOKUWA AKIITUMIA NOKIA YA TOCHI YENYE MFUMO KAMA WAJENEZA NDIO ILIYOTUMIKA KAMA DHAMANA YAKUCHONGEWA JENEZA BABA YANGU KWA MAELEZO NA TAARIFA TULIZOZIPATA KUTOKA KWA NDUGU SURA YA BABA YANGU SIKUIONA IKIWA KATIKA JENEZA WALA RANGI YA JENEZA SIKUIFAHAMU WALA NGUO ALIZOVAA BABA YANGU SIKUZIFAHAMU.
KESHO YAKE TULIPELEKWA ALIPOPUMZISHWA BABA YANGU NA NDIPO TULIPOISHIA KULIONA KABURI TU MVUTANO NA MTAFARUKU MKUBWA SANA ULITOKEA JU YA KIFO CHA BABA YANGU BAADHI YA NDUGU ZANGU WENGINE WALIMTUHUMU MAMA YANGU MZAZI NDIYE ANAYEHUSIKA NA KIFO CHA BABA YANGU.
YULE MAMA WA KAMBO TAYARI ALIKUWA AMEISHAPANDA SUMU ILIYOKARI KWA BAADHI YA NDUGU WALININYOSHEA VIDOLE NA MANENO MAKALI KWA KUONEKANA MIMI NIMKOSAJI KWA BABA YANGU KWAMBA NILIKUWA MWENYE JEURI KWAKE MWENYE KIBURI SIKUMJALI.
MISHALE ILIKUWA NIMINGI KWANGU ILITUA KILA SEHEMU YA MWILI WANGU NA KUNIPA MAJERAHA MAKUBWA.NILIENDELEA KUVUMILIA MAUMIVU NA MATESO NILIYOKUWA NAYO ILIHALI NIKIJUA TU IPO SIKU YATAKWISHA.
NDUGU YANGU UNAYESOMA USHUHUDA HUU BAADHI YA WENGINE NAJUA UTAWAGUSA NA UTAWALIZA LAKINI NATAKA NIKUTIE MOYO YA KWAMBA SHIDA UNAYOPITIA MATESO NA MAUMIVU ULIYONAYO PENGINE UNAPITIA CHANGAMOTO ZA MAMA WA KAMBO NAKUTIA MOYO LIPO KUSUDI JEMA MBELE YAKO AMBALO MUNGU AMEKUANDALIA NA SIKU MOJA UTAKUJA KUWA USHUHUDA KWA WENGINE.
KIKAO CHA UKOO UPANDE WA BABA YANGU KILILIKAA PAMOJA NASI WATOTO WAKE PAMOJA NA MAMA MZAZI NA YULE WA KAMBO KWA AJILI YA KUTAMBUA NA KUFAHAMU MAREHEMU AMEACHA MALI GANI VILIORODHESHWA VITU VYOTE VILIVYOACHWA NA TUKAGAWANYISHWA KILA MTU MALI ZAKE TULIPOFIKA KWENYE HATUA YA NYUMBA NA ENEO YULE MAMA KUMBE ALIBEBA HATI NA NYARAKA ZOTE WAKATI MZEE AKIWA BADO HAJAFA BAADA YA KUULIZWA HATI ZA VIWANJA VIKO WAPI ALISEMA HANA AKAKANA KABISA BAADA YA KUMBANA SANA NA NDUGU ZAKE MAMA WA KAMBO KUMWAMBIA WAONYESHE TU HATI ILIPO NDIPO YULE MAMA AKAITOA.
KIKAO KILICHUKUA MASAA MENGI KILIANZA SAA TATU ZA USIKU NA KUMALIZIKA SAA KUMI NA MOJA ALFAJILI.BAADA YA MAMBO YOTE KUISHA MAMA YULE WA KAMBO ALIWAHI KUONDOKA ENEO LA MSIBA NA KURUDI NYUMBANI
ALIPOFIKA ALIUZA MALI ZANGU ZOTE KABISA NILIZOPEWA MAUMIVU YA MOYO HAYAKUKOMA YALIZIDI KUPAMBA MOTO NINAKUPA HISTORIA HII KWA UCHUNGU MWINGI NA MAUMIVU MAKUBWA.
BAADA YA KURUDI KUTOKA MSIBANI NILIANZA KUFATILIA MALI ZANGU ILI NIZIHAMISHIE KWA MAMA YANGU MZAZI NDIPO NILIPOPATA TAARIFA KUWA MAMA WA KAMBO ALIUZA MALI ZANGU ZOTE.
TULIANZA MAISHA MAPYA NA MAMA YETU MZAZI LAKINI MAISHA YALIKUWA NI YASHIDA TAABU NA DHIKI ILIYOKUWA KUBWA MILO MITATU KWA MAMA YETU MZAZI ILIKUWA NISHIDA UKIPIKWA WALI USIO NA MAFUTA WALA CHUMVI WALA MBOGA NDIO HUO MTAKULA MCHANA NA USIKU KWA KUNYWEA MAJI.BAADA YA KUONA HALI YA NYUMBANI SI SHWARI MAISHA YAMEKUWA MAGUMU NILIAMUA KUJIUNGA NA KUNDI LA WAVUVI WA SAMAKI.
NA MDOGO WANGU ALIANZA KAZI YA KUWATAFUTA WATU WENYE NGUO CHAFU MAJUMBANI MTU ANAKUPA LUNDO LA NGUO UMFULIE ANAISHIA KUKUPA MIA TANO NIMACHOZI NISIOKUJA KUYASAHAU MAISHANI MWANGU.
NILIANZA KAZI YA UVUVI KUTOKA NYUMBANI SAA MOJA JIONI KWENDA VIJIJI VYA MBALI KUTAFUTA SAMAKI NA KURUDI KESHO YAKE ALFAJIRI MKIWA WATU ZAIDI YA KUMI NDANI YA MTUMBWI.
SIKU YA KWANZA NIKAPATA VISAMAKI ANGALAU VILINISAIDIA KUPATA VYA MBOGA NYUMBANI NA VINGINE NIKAENDA KUUZA NIKAPATA ELFU TANO NIKALETA NYUMBANI ILI WAPATE KUNUNUA UNGA WA UGALI.
SIKU YA PILI SIKUPATA KABISA SIKU YA TATU ILINYESHA MVUA KUBWA YA MAWE ILIYOAMBATA NA UPEPO MKALI SANA USIKUWA WA MANANE NIKIWA KATIKATI YA MAJI NIKO JUU YA JIWE NANYESHEWA NA MVUA NILITAFAKARI MOYONI HUKU NINATOKWA NA MACHOZI NIKASEMA BABA USIKU HUU WA MANANE WATU WAMELALA NA FAMILIA ZAO MAJUMBANI WATOTO WAKO NA WAZAZI WAO MAJUMBANI MIMI USIKU HUU NAPATA SHIDA NA TABU YA KUNYESHEWA NA MVUA USIKU WOTE HUU NIKWASABABU YA DHIKI ILIYOKATIKA FAMILIA YETU NIKASEMA MUNGU YATAKWISHA LINI HAYA MATESO NA MAUMIVU NIKIWA NAWAZA HIVYO RADI ZIMEPAMBA MOTO MVUA INAZIDI KUNYESHA NIKO KATIKATI YA MAJI NIKIWA NIMEKAA JUU YA JIWE.
GHAFLA NILIPIGWA NA BUTWAA KUBWA SANA MBELE YANGU NILIONA KAMA MTU AMESIMAMA NIMLEFU SANA SURA YAKE SIKUWEZA KUIONA NIKIWA NIMEKAA HUKU NIMEDUWAA KWA KILE NILICHOKIONA GHAFLA NILIPOTEZA FAHAMU PASIPOKUJUA ASHUKURIWE MUNGU NILIKUWA NIMEKAA KWENYE JIWE LILILO TAMBARALE AMBALO LILINISAIDIA WAKATI WENZANGU WANAKUJA KUNIFATA MAJIRA YA SAA KUMI ZA USIKU KUELEKEA ALFAJILI NDIPO WALIPONIKUTA NIMELALA JUU YA JIWE MKASA HUU HADI LEO HATA MAMA YANGU MZAZI NDIO KAJA KUUJUA JUZI.
....Itaendelea
0 maoni:
Post a Comment