HII NI SEHEMU YA MWISHO YA USHUHUDA WAKE MANONGA CLASSIC KATIKA SIMULIZI YA MAMA WA KAMBO



 
BAADA YA KUWA NIMEKAMATWA NA POLISI KWA KESI AMBAYO ILITENGENEZWA NA MAMA YULE HATIMAE NILIWEKWA NDANI. MPENDWA MSOMAJI WA SIMULIZI HII ASIKWAMBIE MTU SERO SIO PAZURI KAMA UNAVYODHANI SERO NISEHEMU YENYE MIKOSI NISEHEMU YENYE LAANA USIOMBE UKAINGIA SERO. MAMA YULE ALIYENIWEKA NDANI HAKUONDOKA ENEO LA TUKIO BALI ALISUBIRI KUONA NINI KINAENDELEA ALIWAPA TAARIFA RAFIKI ZAKE KWAMBA KAZI AMEIMALIZA.

NIKIWA SERO GIZA NENE BARIDI NA MBU VYOTE VIKAWA VYANGU RAFIKI YANGU KIPENZI ALIKUJA KWENYE GETI ZITO NILILOKUWA NIMEWEKWA NDANI YAKE NILISHANGAA KUONA ANATOKWA NA MACHOZI NIKAMWAMBIA USILIE HAYA NI YA MUDA TU NINAMWAMBIA HIVYO LAKINI MOYO WANGU UNAUMA NA UNAVUJA DAMU YA MAUMIVU NA MATESO.MAMA YULE KUMBE ALIENDA KWA MWENYE KITI AANDIKIWE BARUA YA KUTISHIWA KUWAWA ILI ANIFUNGE JERA NIKAOZEE HUKO NA ALIHONGA HADI PESA ILI ATIMIZE AZIMA YAKE.

YOTE HAYO ALIFANYA KWA SABABU YA MALI YA BABA YANGU AKIJUA KABISA SIKU MOJA NITAKUJA KUIDAI WAKATI HATA WAZO LA KUWA NA MALI YA BABA YANGU SIKUWA NALO KABISA KWA SABABU NILIJUA IPO SIKU MUNGU ATANIPA ZA KWANGU RAFIKI YANGU NDUGU YANGU MALI YA BABA YANGU ILINITESA MALI YA BABA ILINIPA ZORUBA KUBWA MALI YA BABA ILINIFANYA NIIONE DUNIA IMENIELEMEA.BAADA YA MUDA NDUGU ZANGU WALIFIKA AKIWEMO MAMA YANGU MZAZI PAMOJA NA MDOGO WANGU NA SHANGAZI YANGU WALIJARIBU KUNILETEA CHAKULA WALI KUKU LAKINI HAMU YA CHAKULA HAIKUWEPO NINGETOA WAPI HAMU YA CHAKULA NA WAKATI NIKO KWENYE DHORUBA KALI NA SIJUI MWISHO WAKE UTAKUWAJE. MAMA WA KAMBO SITAMSAHAU KATIKA MAISHA YANGU YOTE.

NDUGU ZANGU WALIFANIKIWA KUNIWEKEA DHAMANA NA NIKAWA NIMETOKA TUKAPANGIWA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI. RAFIKI YANGU SIO WOTE WALIOJELA WANAHATIA WENGINE WAMO KWA MAKOSA YA KUSINGIZIWA.ILIFIKIA HATUA MOYO WANGU ULICHOKA NA UVUMILIVU ULINISHINDA MAANA MATESO YALIZIDI NIKITAZAMA NINAKESI YA KUSINGIZIWA NA SIKUJUA KAMA INAWEZA IKANIPELEKA JELA AMA LAA.

NILIJAWA NA ROHO YA KINYAMA NILIJAWA NA ROHO YA KULIPA KISASI MAANA ILIFIKIA MWISHO NIKACHOKA MATESO YA MAMA YULE. NDUGU YANGU KUMBUKA YA KWAMBA UNAWEZA UKAFANYA JAMBO SI KWA KUTAKA ISIPOKUWA KWA KULAZIMISHWA NA MTU.NILIPANGA NIFANYE TUKIO MOJA KATI YA HAYA HATA KAMA NINAKWENDA JELA BASI NIENDE KWA HAKI KABISA.NILIPANGA NIKAMTEKETEZE KWA MOTO WA PETROL USIKU WA MANENO AKIWA NDANI AMELALA LAKINI NIKAJIULIZA NITAANGAMIZA WATU WENGINE WASIO KUWA NA HATIA LAKINI PIA NILIWAZA NIKAKODI WAVUTA BANGI TUKAMVAMIE USIKU WA MANANE NA KUMCHINJA KABISA NILITAKA KUFANYA HIVYO ILI NITIMIZE HATIMA YA KESI ALIYONITENGENEZEA ROHO YA KINYA ILINIINGIA NDANI YANGU.KILA NILIPOKUWA NIKIWAZA KUFANYA HIVYO NAFSI YANGU IKAWA NINZITO SANA SANA.

SIKU YA MAHAKAMANI ILIFIKA NA NIKASOMEWA MASHIKATAKA YA KUTISHIA KUUA NIKAULIZWA NAKUBALI AU NAKATAA NIKASEMA NAKATAA IKAPANGWA TAREHE YA KUSIKILIZWA KESI YULE MAMA AKAULIZWA UNAMASHAIDI AKASEMA ANAO NA MIMI NIKAULIZWA UNAWATU WA KUKUWEKEA DHAMANA KAMA HAKUNA UNAKWENDA MAHABUSU.

NIKIMTAZAMA MAMA YANGU ANALIA NIKIMTAZAMA MDOGO WANGU ANANILILIA USIOMBE YAKAKUKUTA NDUGU YANGU.NAMSHUKURU MUNGU SIKU HIYOHIYO ALITOKEA MTU ANAETUFAHAMU AKANIWEKEA DHAMANA NA NIKAWA NJE KWA DHAMANA.YULE MAMA WA KAMBO KUMBE ALIKUWA HANA MASHAIDI ILIBIDI AFANYE JITIHADA ZA KUNUNUA MASHAIDI SIKU YA KESI ILIPOFIKA TULIKUTANA MAHAKAMANI NA KESI YANGU IKASOMWA MAMA AKAULIZWA UMEKUJA NA MASHAIDI AKASEMA HAPANA AKATOA SABABU ZAKE KESI IKAPANGWA TENA.


SIKU ILIYOFATA ALIKUJA NA MASHAIDI WATATU KAKA MMOJA BIBI MMOJA NA MDOGO WAKE NA MAMA WA KAMBO.TULIINGIA CHUMBA CHA KESI KESI IKASOMWA NA MAMA YULE AKAELEZEA.JALADA LA KESI LILIKUWA LINASOMA KUTISHIA KUUWA LAKINI SIJUI ILIFANYIKA MIUJIZA GANI  JALADA LIKASOMA KESI YA USHIRIKINA MAMA YULE AKASEMA NILIWASHIKA WANAE KICHWANI KWA UCHAWI NILIOKUWA NAO NA WATOTO WAKE WAKAANZA KUUGUA MUENDESHA MASHITAKA AKAMUULIZA WATOTO HADI SASA WANA HALI GANI AKAJIBU WANA HALI MBAYA SANA. BAADA YA YEYE KUMALIZA WAKAFUATA MASHAIDI WAKE KUMBE ALIKUWA AMEWAPANGA JINSI YA KUSEMA ATAKAVYOSEMA YEYE NA WAO WASEME HIVYOHIVYO.

LAKINI MUNGU ALICHAFUA USEMI WAO WAKAPISHANA KATIKA KUTOA USHAHIDI.
WAKWANZA AKASEMA WATOTO WANAHALI NZURI NA WAMEENDA SHULE WAKATI MAMA WA KAMBO ALISEMA WAKO HOI WIKI NZIMA.

ALIPOINGIA NA WAPILI AKAULIZWA UNAMFAHAMU HUYU KIJANA AKASEMA MHESHIMIWA NINAMFAHAMU HUYU KIJANA NIMTOTO WA MUME WAKE NA HUYU MAMA NA NIKIJANA MZURI ASIYE NASHIDA NA AMEZALIWA PALE NYUMBANI HADI ANAKULIA PALE YULE SHAHIDI AKAONGEZEA AKASEMA TENA MIMI MHESHIMIWA NIMELAZIMISHWA TU KUJA KUTOA USHAHIDI AKAINGIA NA WATATU NAYE AKASEMA HUYU KIJANA NAMFAHAMU NI JIRANI YANGU PALE MTAANI AMEKUA NAMUONA NA BABA YAKE NI RAFIKI YANGU HUYU KIJANA HANA TATIZO LOLOTE.USEMI WAO UKABADILISHWA.MAMA YULE ALIPOKUJA MAHAKAMANI ALIKUJA NAO WAKATI WA KESI KUISHA WALIONDOKA KILA MTU NA NJIA YAKE. NDIO LINATIMIA LILE ANDIKO LINALOSEMA WATAKUJA KWA NJIA MOJA NAO WATATAWANYIKA KWA NJIA SABA.

ILIPANGWA TAREHE YA KUSIKILIZWA MIMI IKAFIKA NIKAINGIA KWENYE CHUMBA CHA KUONGOZEA KESI NAYO KESI IKASOMWA NIKAELEZEA ILIVYOKUWA PANDE ZOTE MBILI TUKAWA TUMESIKILIZWA MAAMUZI YAKATOKA KWAMBA YULE MAMA ANADAI KULOGEWA WATOTO WAKE NA SERIKA YETU HUWA HAIAMINI MAMBO YA KISHIRIKINA HUKUMU ILITOKA NIKAONEKANA SINA HATIA NA NIKAACHIWA HURU KABISA.

LENGO LA MAMA YULE ILIKUWA NIKUNIFUNGA JELA NISIONEKANE KABISA URAIANI
BAADA YA KUWA NIMEACHIWA HURU NILIAMUA KUONDOKA NA KUHAMA MKOA WANGU NA KWENDA KUJITAFUTIA MAISHA SEHEMU NYINGINE NDIO KWA MARA YA KWANZA NIKAINGIA JIJI LA DAR NA NDIPO NILIPOKUTANA NA NEEMA YA WOKOVU KANISA MOJA LIKO PALE SINZA EAGT KWA MCHUNGAJI ALIFONCE MWANJALA KWENYE MKUTANO ALIO UHUBIRI DANIEL MOSES KULOLA HAPO NDIPO NIKAKUTANA NA NIKO AMBAE NIKO NA NDIE ALIYEBADILISHA MAISHA YANGU HADI HII LEO MUNGU AMENIBARIKI KIROHO NA KIMWILI MIAKA KUMI YA WOKOVU PIA MWAKA MMOJA NA NUSU WA HUDUMA YANGU.NA MAMA YULE WA KAMBO NILISHAMSAMEHE NA SINA KINYONGO NAE TENA ILA KWA SASA MAISHA YALISHA MCHAPA UCHAWI ALIYOKUWA AKIUFANYA JUU YETU ULIANZA KUMRUDIA NA BAADHI YA JAMII ILIANZA KUMTENGA.


....NA HUO NDIO MWISHO NA HISTORI YA MAISHA YANGU WA MAMA NA WANAWAKE WOTE DUNIANI NINAWAPENDA ILA NAOMBA NITOE USHAURI KWENU KAMA IKATOKEA UKAMPENDA MWANAUME MWENYE WATOTO NA UKAKUBARI KUISHI NAYE NENDA KAWAPENDE WATOTO WAKE PENGINE WANAWEZA KUJA KUWA MSAADA KWAKO.

KWA WABABA WOTE DUNIANI KABLA HUJAMUOA MWANAMKE JUA KWANZA HISTORIA YAKE NA FAMILIA YAKE BABA YANGU ALIOA MWANAMKE AMBAE HAKUIJUA HISTORIA YA FAMILIA YAO KUMBE FAMILIA ILE ILIKUWA INAENDEKEZA USHIRIKINA HATIMAYE SHETANI AKAINGIA KUISAMBARATISHA FAMILIA YETU.

AHSANTENI KWA WOTE MLIOSHIRIKI PAMOJA NAMI KATIKA MKASA HUU WA MAMA WA KAMBO POLENI KWA MLIO UMIA. NADHANI KATIKA YOOTE HAYO NILIYOPITIA MUNGU ALIKUWA ANANITAFUTA NIMTUMIKIE.

                                    -THE END-

Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment