MLEMBA MO KUZINDUA ALBUM KWENYE TAMASHA PEKEE LA KUFUNGA MWAKA JIJINI MWANZA

Gospel Festival:Ni Tamasha Kubwa La Muziki Wa Injili Kuwahi Kutokea Katika Jiji La Mwanza,Kwa Mara Ya Kwanza Litafanyika Jumapili Hii Ya 12/11/2017. 

Tamasha Hilo Litawaleta Pamoja Waimbaji Mahili Wa Nyimbo Zainjili Akiwemo Solomon Mukubwa,Martha Baraka,Hondwa Mathias,Christian Kelvin,Kamodee Mali Ya Mungu,Juliet Busagi,Ben William,Sam D,New Destiny Singers,Havila Gospel Singers,New Version Band,Neema Ng'asha,Upendo Kihayile Na Wengine Wengi.

Tamasha Hilo Litaenda Sambamba Na Uzinduzi Wa Album Ya Mwimbaji Anayechipukia Kwa Kasi Kutoka Jijini Mwanza Mlemba Mo Atakayezindua Album Yake Ya Audio Na Video. 
Sambamba Na Uzinduzi Kutakuwa Na Matukio Mengine Mbalimbali Ya Burudani Ambayo Hayajawahi Kushuhudiwa Katika Tamasha Lolote. 
 
Kiingilio Katika Tamasha Hilo Ni Tsh 3,000/=Wakubwa Na Tsh 1,000/=Watoto Na Ratiba Rasmi Itaanza Saa 6 Mchana Na Tukio Zima Ni Kwenye Uwanja Wa Ccm Kirumba.


Kama ni mwimbaji au mdhamini unayetaka kushiriki kwenye Tamasha hilo,wala hujachelewa wasiliana nasi kwa simu namba:0745018873 au 0717903959.Wote mnakaribiswa!

Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment