NEEMA NG'ASHA KUZINDUA AUDIO NA VIDEO ALBUM YA USILIE TENA DEC 10 CCM KIRUMBA



 
Anafahamiaka kwa jina la Neema Ng'asha mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania anayefanya vizuri katika tasnia hiyo.

Neema anategemea kufanya uzinduzi wa  album yake inayokwenda kwa jina la Usilie Tena jambo hili litakuwa zaidi ya tukio kwani ataua ndege wawili kwa jiwe moja nikiwa na maana kwamba atazindua audio na video album katika siku moja.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku mgeni rasmi akiwa ni John Dominic wakati mgeni wa heshima akiwa ni Angelina Mabula.

Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanategemewa kuhudhulia uzinduzi huo kama wanavyoonekana kwenye picha ya kwanza hapo juu na wengine hapa chini.Orodha itaongezeka
Shughuli nzima inategemewa kufanyika tar 10 mwezi wa 12 mwaka huu 2017 kuanzia majira ya saa nane mchana,na kizuri ni kwamba hakuna kiingilio katika uzinduzi huo ni bure kabisa.Wote mnakaribishwa!

Ili kuzidi kupata taarifa mpya kuelekea uzinduzi huo tafadhali endelea kutembelea mtandao huu wa Promover,kwa mawasiliano zaidi kuhusu tamasha watafte waandaji kwa simu namba:0754228074/0673527249.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment