SASA HUU NDIO FUNGA KAZI,NI KUTOKA KWA GIDEON PAUL YULE MWIMBAJI ANAYEFANYA VIZURI KUTOKA TABORA

 
Yule mwimbaji wa nyimbo za injili anayevuma kwa kasi kutoka mkoani Tabora anayeitwa Gideon Paul amekuja tena na hii kubwa kuliko inaitwa 'AKUKUMBUKE'.Wimbo huu ndo umebeba album yake ya kwanza na ya pekee hadi sasa.

Akukumbumbe ni wimbo uliomtambulisha Gideon katika ulimwengu wa muziki wa injili nchini Tanzania na kumpa umaarufu mkubwa mkoani Tabora yalipo makazi yake.Wimbo huu ameshirikiana na mwimbaji anayeitwa Daniel Thomas yule alivuma na wimbo wa ibada njema inaanzia nyumbani.

Wimbo huu umerekodiwa katika studio za KapstoneProduction kwa mikono ya producer Baraka Richard(BK).Hakika ukiusikia wimbo huu lazima ubarikiwe na wala hutojuta kuupakua.

Gideo Paul yupo tayari kabisa kushirikiana na mwimbaji yoyote ndani na nje ya nchi pia yupo tayari kwa mialiko ndani hata nje ya nchi,kama ungependa kuwasiliana naye mtafte kwa simu namba:0762700762/0686183714.

-Karibu sasa uusikilize wimbo wa Akukumbuke:
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment