Huyu ni Mpe Mwalupogo muimbaji kutoka Mbeya ambaye aliibuka mshindi wa kipangele cha muimbaji bora wa kike 2018 katika tuzo zilizotolewa na radio uhai fm ya mkoani Tabora.
'Naitwa Mpe
Mwalupogo nimezaliwa tukuyu eneo la itete nimeanza kuimba toka mdogo nikiwa darasa la 3 nikajiunga na uwaki nilikuwa mdogo lakini nilipendwa
na mwalimu wangu kwa sababu ya sauti yangu ya pili ukawa mwanzo wa kuanza huduma ya
kuimba.
Nilipofika secondary
niliendelea na UKWATA
Katika maisha yangu
yote sijawahi ishi bila kujiunga na kwaya au kikundi cha kusifu na kuabudu
popote ninapoenda haijalishi ni wapi.
Nilipo jiunga chuo
kikuu 2016 nilijiunga na kikundi cha USCF tawi la TABORA hapo ndipo
nilipoanzia kuimba kama mwimbaji binafsi.
Nime record nyimbo
zangu mbili 2018 ambazo ni
1.unaweza
2. Wewe ni mwema
Namshukuru Mungu hizi
ndizo zimenipa ushindi kuwa mwimbaji bora wa kike Tabora 2018.
Kwann wimbo
unaweza:
Huu niwimbo unao husu
maisha yangu mwenyewe
Namshukuru Mungu kwa
matendo makubwa alionitendea simba dubu hawakunidhuru
Mfano 1: nilipokuwa
darasa la 2 nilizama ziwani
2. Nilipokuwa form 4
mwaka 2013 niling'atwa na nyoka nusu ya kifo mwezi mzima nipo kitandani nilipona
kwa maombi.
3. Nilipokuwa form 6
niliumwa mwezi mzima na huku nina mtihani wa mwisho,nilipona week 2 kabla
ya mitihani.
Nipo tayari kwa mwaliko popote.
0 maoni:
Post a Comment