Padri wa ngazi ya juu
katika makao makuu ya kanisa Katoliki ya Vatican anayetuhumiwa kukiri
kumtongoza mtawa amejiuzulu.
Taarifa hiyo imetangazwa jana na Vatican. Padri
huyo raia wa Austria Hermann Geissler amejiuzulu kama mmoja wa viongozi wa juu
katika taasisi inayoshughulikia mafundisho ya imani ambayo inafuatilia maadili
ya kikatoliki.
Taarifa ya Vatican imesema Padri huyo ameamua kuchukua uamuzi wa
kujiuzulu ili kuzuia uharibifu ambao umeshafanywa kwa waumini na jamii yake.
Mchakato wa sheria za
kidini zinazohusu adhabu uliofanyika 2014 ulimpa onyo padri Geisler baada ya
mtawa wa zamani Doris Wagner kumtuhumu kuwa na tabia zisizofaa wakati wa
kuungama.
Mtawa huyo alisema
aliwekwa kwa masaa mengi akiwa amepiga magoti huku padri huyo akimueleza kwamba
anampenda kimapenzi na hata kama hawaruhusiwi kuoana wanaweza kutumia njia
nyingine.
Source:DW
0 maoni:
Post a Comment