Anaitwa Saimon Ngwena Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka mkoani Tabora ambaye aliweza kuibuka mshindi wa kipengele cha muimbaji bora wa kiume 2018 katika tuzo zilizotolewa na radiou uhai fm ya mkoani Tabora.
Saimon Ngwena anayo album moja inaitwa Umenivusha ambayo ipo sokoni hadi sasa ikiwa imesheheni nyimbo zenye ubora wa hari ya juu.
Akizungumza na Promovertz.com Saimon ameeleza historia yake ya uimbaji kama ifuatavyo:
'Naitwa Saimon Ngwena mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania,namshukuru Mungu kwa kuendelea kunitumia katika kuujenga ufalme wake kwa njia
ya uimbaji,nilianza kuimba tangu nikiwa mdogo sunday school, Upendo
kwaya,Praise team, kwaya ya vijana, Utumishi kwaya na Band mbali mbali
nyumbani mkoani Tabora katika kanisa la f.p.c.t kiloleni Tabora.
nikiwa chini ya
mchungaji wangu baba yangu wa kiroho Pst. Peter Shani.Mungu ni mwema
siku hadi siku Mungu hakuniacha 2009 nilianza kujitegemea kiuimbaji kuwa
mwimbaji binafsi,2010 nilingia studio nikarecod album yangu ya kwanza inayo
kwenda kwa jina la Umenivusha ambapo album hiyo ilikuja kukamilika 2012
kutokana na changamoto ya kipesa ambayo ilikuwa ya kuunga unga.
2013 nilifanya
video ya album hyo ikaja kukamilika 2014.na 2015-2017 nikawa naendelea
kuzunguka kufanya huduma, na 2018 Niliweza kuachia single yangu ya wimbo wa
Ebeneza ambao kwa sasa unafanya vizuri sana na wimbo huo umeweza kunifanaya
kuwa mshindi mwimbaji bora wa kiume kupitia Radio uhai Fm 94.1 Tabora
Tumeingia mwaka mpya 2019 Mungu wetu niwa viwango kila siku..hata mimi huduma
yangu itakuwa ya viwango tena zaidi'
Kwa mawasiliano zaidi mpigie Simon kwa simu namba:+255658 212 664
Kwa mawasiliano zaidi mpigie Simon kwa simu namba:+255658 212 664
0 maoni:
Post a Comment