HAPPY BIRTHDAY THE SUPER BLOGGER JACKTAN MSAFIRI



Leo tarehe 21/11 ni kumbukumbu ya miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake Jacktan Msafiri ambaye ni mwandishi mkuu(Chief Blogger)wa mtandao huu wa PROMOVER.COM

PROMOVER.COM inatambua na kupongeza mchango mkubwa wake Jacktan Msafiri katika masuala yote ya injili na habari mbalimbali.

Katika kusherekea siku yake hii muhimu Jacktan Msafiri ambaye pia ni Mtangazaji wa kituo cha redio ya kikristo cha jijini Mwanza kinachoitwa kwaneema fm,ameyaandika haya katika ukurasa wake wa facebook

'Tarehe ya leo miaka mingi iliyopita niliingia rasmi duniani.Nimejifunza mengi na ninaendelea kujifunza jipya kila kukicha.

Nawashukuru wote mliochangia mimi kufika hapa,wote mlionisaidia kwa namna yoyote ile familia,rafiki ndugu na wengine wote.

Safari bado ni ndefu lakini pia nilikotoka ni mbali.Ujumbe wangu leo kwa wote ni kwamba "Mungu wetu ni mwaminifu lakini ana upendeleo" tufanye kazi kwa bidii tukimtegemea yeye naye atatulipa kwa namna ile ile.

Hpy bday to me,natamani miaka mingine 50 hapo ntakuwa nimemaliza deni langu duniani.Nawatakia siku njema'

Tunamtakia heri na fanaka Tele mwenzetu katika maisha yake yote.Happy birthday Jacktan Msafiri
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment