HIKI NDICHO KILICHOMSABABISHA WALTER CHILAMBO KUINGIA KWENYE MUZIKI WA INJILI


Walter chilambo sio jina geni nchini Tanzania,alijizolea umaarufu mkubwa sana baada ya kushinda mashindano makubwa ya kusaka vipaji yanayoitwa Bongo Star Search(BSS).

Baada ya kushinda katika mashindano hayo Walter aliingia rasmi katika muziki wa bongo fleva ambapo aliachia nyimbo mbalimbali zilizowavutia wengi.

Lakini Walter Chilambo amekaa kimya sana kwa takribani miaka miwili bila kuachia wimbo mpya zaidi ya kurudia nyimbo za wasanii wengine wa bongo fleva yaani cover,ambazo hata hivyo zilimpa umaarufu kwani amekuwa akizifanya kwa ustadi mkubwa sana.

Siri imekuja kufichuka kwamba ukimya wake ulisababishwa na maamuzi magumu aliyokuwa akiyafikilia maamuzi ambayo ni sahihi na yenye kupongezwa sana.

Maamuzi hayo ni ya kugeuka na kumwimbia bwana,ndio Walter Chilambo ameanza rasmi kuimba nyimbo za injili yaani gospel ambapo anaamini waimbaji wenzake wa bongo fleva wataiga uamuzi wake.

Je! ameokoka kabisa au anaimba tu kumtukuza mungu?majibu yote yako kwenye video hii hapa chini alipofanya mahojiano na HZB TV ambapo pia kazungumzia ugumu alioupata wakati akifanya video yake mpya ya Asante.


Video mpya yake Walter Chilambo 'ASANTE' imeendelea kujizolea umaarufu kutokana na ukweli kwamba video hiyo imetengenezwa katika ubora wa hali ya juu kuanzia rangi mazingira na hata uimbaji kwa ujumla,Itazame hapa video hiyo.
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment