PAPA FRANCIS AMTUNUKU MTANZANIA TUZO YA HESHIMA



KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Fransisko amemtunuku tuzo ya heshima aliyekuwa mkuu wa Idara ya afya mstaafu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Daktari Fredrick Kigadye kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa kanisa Katoliki.

Mwadhama, Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kwa niaba ya Baba Mtakatifu Fransisko alikabidhi tuzo hiyo kwa daktari Kigadye jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika baraza la maaskofu.

Baada ya kukabidhi tuzo hiyo Kardinali Pengo alisema amejisikia furaha kwa tendo hilo kubwa katika kanisa lao hapa nchini la daktari Kigadye kupewa tuzo hiyo.

“Daktari Kigadye ametusaidia sana katika masuala ya Pasada kwa hiyo nina sababu ya ziada ya yale yaliyoongelewa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa tukio hili. Ni shukrani kubwa kwa Baba Mtakatifu Fransisko aliyeridhia ombi la maaskofu kutoa hii hati pamoja na nishani.Hati ikitolewa na Mwenyezi Mungu mambo mengine ni ziada,” alisema Pengo.

Naye daktari Kigadye alitoa shukrani zake kwa Mungu, Baba Mtakatifu Fransisko na kwa maaskofu wote waliochangia jambo hilo kufanikiwa.
 -Daktari Fredrick Kigadye
“Asante kwa Mwenyezi Mungu kwa uhai na majaliwa yote kwangu na wote walioshiriki katika malezi yangu hadi kufikia siku ya leo kihistoria,” alisema daktari Kigadye.

Kwa upande wake rais wa Maaskofu Katoliki Tanzania, Tarcisius Ngalalekumtwa alimtaka daktari huyo asijisifu wala kujivuna kwa kuwa jambo hilo lililofanyika ni kazi ya Mungu.
 
Tuzo hiyo ‘Bene Merenti’ maana yake ikiwa ni ‘kwa yule anayestahili’ ilipokelewa kwa furaha na katibu mkuu wa TEC, Padri Raymond Saba.

-Kutazama picha za hafla hiyo,>>Bonyeza HAPA 
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment