KANISA LA MENNONITE NYEGEZI KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA INJILI


Kanisa la Mennonite lililopo Nyegezi  jijini mwanza,linawakaribisha  wananchi wote katika mkutano mkubwa wa injili unaotarajiwa kufanyika kwa wiki nzima kuanzia jumatatu ya tar 5 dec hadi jumapili ya tar 11 dec 2016.

Mkutano huo wa injili utafanyika katika viwanja vya kanisa hilo linalopatikana pembezoni ya barabara iendayo chuo kikuu cha SAUT kwenye eneo maarufu liitwalo Bondeni.

Mchungaji mwenyeji wa mkutano huo Mch Zablon Mtende kwa kushirikiana na mchungaji kutoka jijini Arusha Pastor Davis Tumaini,watafanya maombezi kwa wagonjwa na wote wanaosumbuliwa na vifungo vya shetani watafunguliwa.

Masomo mbalimbali ya kukujenga yatafundishwa kwa wote,njoo tuzifunze njoo upokee Baraka na uponjaji.Kumbuka hakuna kiingilio ni Bure kabisa.

Waimbaji mbalimbali watahudumu katika mkutano huo mkubwa wa injili kama vile: Betty Lucus,Masanja wa Arusha,Yohana Band,Revival Band,AIC Makongoro vijana choir wanakekundu,AIC Nyakato choir,AIC Mkolani choir,Mennonite Nyegezi choir(Shilo Band),Mennonite Mabatini choir,Mennonite Mabatini,Mennonite Kirumba choir,na bila kuwasahau wenyeji Mennonite Nyegezi choir wana wa uamsho na wengine wengi watakuwepo.

Usikose mkutano huu,kumbuka ni pale kanisani Mennonite Nyegezi Bondeni kuanzia tar 5-11 dec mwaka huu na mkutano huo utakuwa ukianza majira ya saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni.Hakuna kiingilio ni bure kabisa

Woote mnakaribishwa!
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment