Huu ni mwendelezo wa mikesha mikubwa ya kila mwezi ambayo hufanywa na kanisa hilo,ambapo katika mkesha wa kesho utakuwa maalumu kwaajili ya kuliombea taifa na viongozi wake,kuomba amani,kuombea wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani,kuombea wafanyabiashara na watu mbalimbali wenye mahitaji ikiwa ni pamoja na maombi na maombezi ya kuunguliwa kwa wote.
Akiongea na PROMOVER.COM mchungaji kiongozi wa kanisa la Kwaneema Mch Philipo Stanslaus amesema mkesha huo hauna kiingilio ni bure kabisa kwa kila mmoja hivyo kuwataka wanakanda ya ziwa na nje ya mipaka yake kufika kwa wingi katika mkesha huo ili kupokea baraka hasa ikizingatiwa mikesha hiyo hufanyika mara moja kwa mwezi.
Waimbaji mbalimbali watakuwepo kwenye mkesha huo wakiongozwa na wenyeji wao Kwaneema Band na Kwaya ya vijana ya TFE,Bila kusahau mwimbaji mahili wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza anayeitwa Betty Lucus.
-Betty Lucus |
Njoo ufunguliwe njoo uwekwe huru,walete wenye shida na magonjwa mbalimbali watafunguliwa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kanisa la TFE kwaneema piga simu hizi:
Mch:Paul Chaba-0756 373 008
Mch:Philipo Stanslaus-0762 695 094
0 maoni:
Post a Comment