FAHAMU JINSI YA KUWAPIGIA KURA KIHAYILE GROUP KWENYE TUZO ZA KENYA

Kihayile group ni moja kati ya kikundi cha muziki wa injili kutoka jijini mwanza kilichochaguliwa kushiriki katika tuzo za XTREEM AWARDS KE 2016 za nchini Kenya.

Hizi ni tuzo kubwa kabisa za injili nchini humo baada ya zile za GROOVE AWARDS,ambapo watanzania kadhaa wamechaguliwa kushiriki katika tuzo hizo ambazo zitatolewa Nov4-16Nov ukumbi wa Kenya national Theatre mjini Nairobi nchini Kenya.

Pengine unaweza kuwa mmoja kati ya wale ambao wangependa KIHAYILE GROUP waibuke na tuzo hizo na unapenda uwapigie kura,basi shaka ondoa PROMOVER.COM inakuletea njia za kuwapigia kura kiyahile na watanzania wengine katika tuzo hizo.

Kama upo nchini Kenya Tuma sms yenye neno KIYAHILE GROUP kwenda namba 21921.njia hiyo pia inaweza kutumika kwa nchi nyingine japo kuwa ina ugumu kidogo kutoka na na vifurushi vya mitandao kutoruhusu njia hiyo.

Njia nyepesi kwa nchi nyingine kupiga kura,ni kwa kufuatilia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za waandaji wa tuzo hizo yaani XTREEM AWARDS kisha unakomenti neno KIYAHILE GROUP kwenye machapisho ya waandaaji hao.

Hakikisha umekomenti kwenye ukurasa rasmi wa XTREEM AWARDS kwenye facebook,instagram na twitter ukihakikisha pia umewatag.Kurasa hizo zina majina yafuatayo kama inavoonekana kwenye picha hapa chini:
Ukitaka kuwapigia kura kwa kucomment tafadhali fuata mfano huu hapa chini,hii ni kwa instagram,facebook na twitter ya waandaaji wa tuzo hizo.fanya hivi mara nyingi uwezavyo kila siku
   

 -Kuwapigia kura kihayile kwa njia ya instagram bonyeza>>VOTE FOR KIHAHIYE GROUP ON INSTAGRAM

-Kuwapigia kura Kihayile Group sasa kwa njia ya facebook,bonyeza>>VOTE FOR KIHAYILE GROUP ON FACEBOOK

-Kuwapigia kura Kihayile Group kwa njia ya twitter,bonyeza>>VOTE FOR KIHAYILE GROUP ON TWITTER

Ukiachilia mbali Kihayile Group,pia wapo watanzania wengine waliochaguliwa katika tuzo hizo,kuwafahamu ni akina nani hao bonyeza>>HAPA

-Huu ni mmoja kati ya wimbo wao Kihayile Group 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment