MTOTO MWENYE WAZAZI WATATU AZALIWA MEXICO























Mtoto wa kwanza aliyetengenezwa kwa kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu amezaliwa,jarida la kisayansi New Scientist limetangaza.


Wakikiuka rasmi amri mpya aliyoitoa papa Francis hivi karibuni, wataalam wa tiba wamefanikiwa kuingia maabara na kutengneza mtoto wa kiume mwenye chembe (DNA)kutoka kwa mama yake,baba yake, pamoja na jeni za mfadhili.


Madaktari wa marekani walichukua hatua hiyo kuhakikiha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali ya jeni ambayo mama yake kutoka Jordan anabeba katika mwili wake.


Wataalam wanasema kuwa,hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyingine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida.


Lakini wameonya kuwa, uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ‘Ufadhili wa Mitochondrial’unaitajika.
 

Mitochondrial ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini.


Baadhi ya wanawake hubeba jeni  zilizo na kasoro na wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.


Wanasayansi waliohusika katika shughuli hiyo,walsafiri hadi Mexico kwa sababu huko hakuna sheria za kuzuia shughuli kama hiyo ya kimatibabu.


Walichukua sehemu muhimu za chembe za kinasaba (DNA)kutoka kwa yai la mama,na DNA ya mitochondria kutoka kwa yai la mfadhili  na kuunda yai lenye afya ambalo lilitungishwa mbegu kutoka kwa baba.


Matokeo yake ni kuzaliwa kwa mtoto mwenye asilimia 0.1 ya DNA kutoka kwa mfadhili na jeni nyingine zote,zinazoamua sifa kama vile rangi ya nywele na macho kutoka kwa mama na baba.


 

Lakini mchezo huo wa kisayansi tayari umekwaa kisiki kwa kuwa licha ya kanisa katoliki kuupinga na kusababisha baadhi ya mataifa  ikiwemo  marekani kuupiga  marufuku, papa Francis ameamua kutengeza amri  mpya inayopiga marufuku uhandisi wa jeni.


Kwa muda mrefu, kanisa Katoliki lilipinga shughuli ya uhandisi jeni na ni kutokana na nguvu zake,mataifa kadhaa duniani ikiwemo Marekani,yalipiga marufuku uhandisi huo na hilo lilipelekea wanasansi wa Marekani kubeba wazazi watatu hadi nchi ya Mexico na kufanyia shughuli hiyo huko Dk John Zhang,Mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya New Hope Fertility Centre jijini New York City,amesema yeye na wenzake walitumia njia hiyo kupata viineitete vitano lakini wakastawisha kimoja tu.

 















Chanzo:Gazeti la Nyakati
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment