WAKRISTO NCHINI KOREA KASKAZINI HUABUDU KWA KUJIFICHA,WAKIBAINIKA WANATEKETEZWA KWA MOTO NA KUCHINJWA KAMA WANYAMA




Lile neo la Bwana Yesu la “ikiwa wameutenda hivi mti mbichi itakuwaje kwa mti mkavu”linatimizwa kwa kasi kwa wanaoungoja ufalme wa mbinguni katika maeneo mbalimbali duniani.


Hii ni pamoja na mateso ambyo maelfu ya wakristo yakiwemo mauaji ya kuteketezwa kwa moto,kuchinjwa kama wananyama na kupigwa risasi,wanaendelea kuyapata.


Korea kaskazini ni baadhi ya mataifa yanayodaiwa kuwa na rekodi kubwa ya kuhuskika katika mateso hayo kwa wakristo nchini humo kwa muda mrefu sana,utafiti umebaini.


Matokeo ya utafiti yaliyotolewa na shirika linalohusika na masuala ya uhuru wa kidini kutoka UK wiki iliyopita,inaonesha kuwa wakristo katika taifa hilo wamekuwa katika mateso ya kiutumwa,kubakwa na kuuawa.


Kwa mujibu wa mtandao wa habari za kikristo duniani ambao ulisambaza matokeo ya utafiti huo,imani za kidini ukiwemo ukristo zimekuwa tishio kubwa kwa wakuu wa taifa hilo na iwapo mtu yeyote atabainika kujihusisha nazo inampasa mateso makubwa.


Inaelezwa kuwa wakristo wengi nchini humo wamekuwa katika mateso makubwa kutokana na kutokuwa na radhi na utawala wa kibeberu na kupinga mapinduzi dhidi ya imani yao.


Utafiti huo umeendea kubainisha kuwa wakristo wamekuwa wakisurubiwa juu ya misalaba kwenye moto,kukatwa vichwa,kuburutwa na kukanyagwa miguu.


Pia sera ya nchin hiyo kuhusu ushirikishwaji,watu wote wenye undugu au urafiki na wakristo wanatiwa hatiani kwa kupelekwa gerezani bila kujali wanauamini ukristo au laa.


“Hata raia wa Korea kaskazini ambao wamekimbilia nchini China na ambao ni wakristo au wanakubali kuwa wakristo wanarudishwa nchini kwao na kupelekwa kwenye makambi ya magereza ya kisiasa” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

 
Hadi sasa idadi ya wakristo nchini Korea Kaskazini kwa mujibu wa takwimu  za Cornerstone Ministries International ni kati ya 200,000 na 300,000 huku zile za kiserikali zikisema ni 13,000.


Hadi sasa wakristo nchini humo wametakiwa kuendesha ibada kwa siri vinginevyo wasubiri kwenda kwenye makambi ya mateso.


Wakati huo huo,mamia ya  wabunge,wanasheria chini ya umoja wao wa IPPFoRB,wawawikilishi wa makanisa na wale wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchi mbalimbali duniani,wamejichimbia nchini Berlin Ujerumani huku ajenda kubwa ikiwa ni kupinga mateso na unyanyasaji unaofanywa kwa watu juu ya imani zao za kidini.


Mkutano huo ambao ulifanyika mwezi uliopita katika bunge la Ujerumani na kufunguliwa na kansela wa taifa hilo,Angela Merkel, unafanana na ule uliofanyika katika jiji la New York mwaka uliopita.

  



Chanzo:Gazeti la jibu la Maisha
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment