
Serikali Imesitisha Shughuli Iliyokuwa Ikiendeshwa Na Mchungaji Getrude Lwakatare Ya Kuwalipia Faini Wafungwa Walioko Magerezani Hadi Hapo Utaratibu Mwingine Utakapotolewa.
Mpango Huo Unaofanywa Na Lwakatare Kwa Kushirikiana Na Mwenyekiti Wa Taifa Wa Bodi Ya Parole,Augustine Mrema Tayari Umewezesha Wafungwa 78 Kutoka Magerezani Baada Ya Kuwalipia Faini Inayofikia Shilingi Milioni 25.
Mkuu Wa Magereza Mkoa Wa Dodoma, Bw: Antonio Kilumbi Amesema Amepata Maelekezo Ya Kusitishwa Kwa Mpango Huo Kutoka Ngazi Ya Juu Ya Jeshi Hilo.Amesema wananchi wengine bado wana uwezo wa kuwalipia faini hiyo ndugu zao.
Kwa
Upande Wake Bw:Augustine Mrema Amesema Mpango Huo Ulilenga Kupunguza Msongamano
Magerezani Na Kuipunguzia Serikali Gharama Za Kuwahudumia Wafungwa.
0 maoni:
Post a Comment