MCHUNGAJI AWANYWESHA WAUMINI DAWA YA CHOONI AKIDAI INAWAPONYA MAGOJWA YAO



 



Je!uliipata ile taarifa ya mchungaji huko afrika kusini kupulizia waumini dawa ya kuua mbu machoni akidai ni tiba? kama uliipata hiyo basi kuna ripoti mpya kutoka huko huko afrika ya kusini ambapo wakati huu sasa mchungaji anawanywesha waumini dawa ya kuua bakteria aina ya Dettol ambayo nchini Tanzania hutumika zaidi kusafishia chooni.

Mchungaji  maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK SpiritualChristian lililopo Makgodu,Limpopo,AfrikaKusini amewashangaza watu kwa kitendo cha kuwanywesha  Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu.

Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.

“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,”  – Mchungaji.

Pia alisema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa

“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na kufariki.

 “Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”
Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata.

Kama ulipitwa na ile ya dawa ya mbu ipitie sasa hapo chini:


Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment