HATIMAYE WIMBO MAALUMU WA KISWAHILI KWAAJILI YA KRISMAS UMEPATIKANA,USIKILIZE HAPA



Tukiwa tunaelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka za krismas na mwaka mpya kuna vingi ambavyo huashiria kuwa sikukuu hizo zinakaribia lakini burudani ya muziki ni moja kati ya viashiria vikubwa vya sikukuu hizo.

Tatitizo limekuwa kwamba kwa miaka mingi sasa hakuna nyimbo nyingi maarufu za kiswahili za injili zinazoelezea kuhusu sikukuu hizo,taarifa nzuri ikufikie kwamba hatimaye wimbo mzuri maalumu kwaajili ya krismas umepatikana.

Wimbo huo mpya kabisa ambao kwa mara ya kwanza tunautambulisha kupitia tovuti hii,unaitwa 'Emmanuel(Amezaliwa Mwokozi)'ukiwa umeimbwa na waimbaji kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania.

Waimbaji hao ni kundi maarufu la waimbaji linaloitwa Kihayile group wakiwa wameshirikiana na Hondwa Mathias pamoja mwimbaji YZ ukiwa umerekodiwa AB records.

Karibu sasa uusikilize wimbo huo kisha usambaze kwa rafiki zako kisha wote mbarikiwe na kuburudika katika msimu huu wa sikukuu.
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment