Shule
zimefunguliwa nchini Swaziland chini ya agizo jipya la serikali kufunza somo la
dini ya kikristo pekee, hatua iliokosolewa kwa kuwa inakataa kuheshimu dini
nyengine kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Wizara
ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala
hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.
Kimemnukuu
Sahid Matsebula, raia muislamu ambaye anafanya kazi msikitini karibu na mji
mkuu wa Mbabane, kwamba sera hiyo huenda ikazua wasiwasi wa kidini katika
ufalme huo.
''Serikali
ina mpango gani kwa watoto wetu ambao sio Wakristo? Watafunzwa kitu kimoja
nyumbani na kufunzwa kitu chengine shule''.
Sera
hiyo mpya inajiri baada ya raia kulalama kwamba wahamiaji wa bara Asia na wale
wa kiislamu wamekuwa wakiingia nchini humo hatua iliolazimu bunge kubuni kamati
ya kuchunguza mwaka uliopita, AFP imeripoti.
Wahamiaji
wengine tayari wamerudishwa makwao na waziri wa biashara Jabulani Mabuza
ameambia bunge kwamba sheria itakayowazuia wahamiaji kuanza biashara nchini
Swaziland imeanza kubuniwa.
Stephen
Masilela, rais wa baraza la makanisa nchini humo ameunga mkono mtaala huo mpya.
''Ukristo
ndio msingi wa kujengwa kwa taifa hili''.
Mfalme Mswati 111 wa taifa la Swaziland |
Taifa
la Swaziland linaloongozwa na mfalme Mswati wa tatu tangu 1986 lina idadi ndogo
ya waislamu.
CHANZO:BBC
0 maoni:
Post a Comment