KAMA UPO MWANZA KONGAMANO HILI LISIKUPITE,NI KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA KWA MCH KULOLA



 
Ni Kongamano na mkutano mkubwa wa injili kufanyika jijini Mwanza ukiletwa kwako na kanisa la EAGT Lumala Mpya chini yake mtumishi wa Mungu Mchungaji Dkt Daniel Moses Kulola.

Mkutano huo ni mkubwa na wa aina yake kuwahi kutokea katika jiji la Mwanza ambapo kutakuwa na ugeni mkubwa wa mchungaji kutoka nchini marekani anayeitwa Matias Rojas akiwa na timu yake.

Kongamano hilo litafanyika katika viwanja vya Sabasaba ilemela jijini Mwanza kuanzia tar 27/8/2017 hadi  1/10/2017 Saa 9 mchana hadi saa 12 na nusu jioni.

Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili watakuwepo kuhudumu katika kongamano hilo akiwemo Ambwene Misuli ya Imani kutoka jijini Dar es salaam,Joseph Rwiza kutoka Dodoma,Mbilikimo watatu kutoka Arusha,Sam D kutoka Mwanza,Sarah Akram,Cecilia Mashikolo,Ndageji Mitagato,Havilla singers,Revival Aic Choir na wengine wengi.

Walete wagonjwa na wenye shida mbalimbali,wataombewa na kuwekwa huru kabisa.Kwa Mawasiliano zaidi mpigie Mch Dkt Daniel Kulola kupitia simu namba:0767749040.Watu wote Mnakaribishwa!

Bonyeza play hapo chini kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo pamoja na kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa ujumla.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment