GOODLUCK GOZBERT AINGIA MKATABA NA MAXBURUDANI,SASA ALBUM YAKE UTAIPATA KWENYE VITUO VYA MAXMALIPO

 
Mwimbaji anayefanya vyema katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na Afrika mashariki Goodluck Gozbert, ameingia mkataba rasmi na kampuni ya Maxcom kupitia mfumo wao mpya wa kusambaza kazi za wasanii ndani na nje ya Tanzania uitwao MAX Burudani.

Baada ya timu ya habari ya gospomedia.com kukutana na mwimbaji huyo alifunguka mambo kadhaa kuhusu kuingia mkataba huo ambao kwa upande wake ameona ni fursa kubwa katika kutangaza na kuuza kazi zake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania huku akitilia mkazo kusudi lake kuu la kuitangaza Injili kupitia muziki na kuziponya nafsi za watu wengi duniani kote.

“Nimeingia mkataba na kampuni ya Maxcom yenye mfumo mpya wa usambazaji wa kazi za muziki na filamu kwa wasanii uitwao Max Burudani ambapo mpaka sasa ninapozungumza tayari mfumo huo umeshaanza kufanya kazi na Tarehe 1 Januari 2018, album yangu mpya ya Shukurani Itakuwa Inapatikana nchi nzima, ambapo kampuni hii ina mawakala zaidi ya elfu kumi na sita kwa mikoa ya Tanzania, Ni mfumo rahisi ambao utawawezesha watu wa Mungu kupata albamu yangu mpya kupitia vituo vya Max Malipo nchi nzima kuanzia tarehe 1 January 2018.

Kwa kipindi cha mwezi mmoja tutaanza na Tanzania lakini baada ya hapo tutaenda pia nje ya mipaka ya Tanzania ambako huduma za Maxmalipo zinapatikana” – alisema Goodluck Gozbert.

Hakika hii ni habari njema katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania ambapo kupitia mwimbaji Goodluck Gozbert milango ya mafanikio imeanza kufunguka na ni imani yetu kwamba waimbaji wengi wa muziki wa Injili watanufaika na mfumo huu ambao si tu utaboresha maisha yao kiuchumi lakini pia utakuza huduma zao na kutangaza neno la Mungu kwa mataifa mengi kupitia muziki wa Injili.

Kama hujapata nafasi ya kutazama video na kupakua wimbo unaoendelea kufanya vizuri uitwao Shukurani, nakukaribisha sasa kuitazama video hii na kupakua wimbo huu na ni hakika utabarikiwa.  
Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Goodluck Gozbert kupitia:
Simu/WhatsApp:+255 655 212 720 au +255 654 276 560​⁠​ 
Facebook:Goodluck Gozbert 
Instagram:@goodluckgozbert 
Youtube:Goodluck Gozbert 
Twitter:@goodluckgozbert 
Website:www.goodluckgozbertministry.com

Source:GospoMedia.com
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment