TAZAMA VIDEO MPYA:SAYUNI MRITA | YESU AMEFANYA


Kwa mara nyingine tena muimbaji wa nyimbo za injili kutoka mkoani Morogoro anayeitwa Sayuni Mrita anatuletea zawadi ya video nzuri kabisa.

Ni video ya wimbo wake mpya unaooitwa Yesu Amefanya unaoelezea ukuu wa Mungu katika maisha ya mwanadamu.

Video hii imeongozwa na kampuni ya Brayance Works chini ya Director Hassan Mbangwa, Muziki ukiwa umetengenezwa na Barnabas Nason akishirikiana na Kingson na Papaa Denilson.
Akizungumza na Promovertz.com Sayuni amesema:
Ujumbe katika wimbo huu ni kuwa kuna wakati wa Mungu kwa kila jambo chini ya jua.Ujumbe wa wimbo huu unatoka Mhubiri 9:11 “…si wenye mbio washindao katika michezo,wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote”. Wakati wa Mungu unapofika, 

Mungu hubadilisha hali ya mtu na kuifanya nzuri (Mhubiri 3:11 – Mungu hufanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake…). Kwa aliyekata tamaa kuwa mambo hayaendi anavyopenda, wakati wako utafika tu na mambo yako yatabadilika na kuwa sawa. 

Mungu ni mwaminifu daima.Baadhi ya shuhuda kwa waliosikiliza na kuona video ya wimbo huu: “...nikianza kuitazama video hii, sitamani kuacha kuitazama. Naweza kuitazama mara nyingi bila kuchoka... Hakika ni wimbo wa tofauti sana...”

Mziki wa wimbo huu umetengenezwa na Barnabas Nason wakati producers wakiwa Kingson na Papaa Denilson.  *Video imefanywa na Brayance Works chini ya Director Hassan Mbangwa.* 

Ili kuendelea kufualitila huduma hii na kwaajili ya mialiko unaweza kumpata  Sayuni Mrita kwa mawasiliano yafuatayo:

Intagram – sayuni_mrita, 
Youtube na Facebook –Sayuni Mariki-Mrita. 
Simu/WhatsApp: +255 686 815 115
Karibu sasa utazame wimbo huo:
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment