ASKOFU MOKIWA ATAKA SERIKALI ICHUNGUZE TAASISI ZA DINI ZA WATU BINAFSI

               
Ni Moja kati ya habari kubwa iliyopewa kipaumbele kwenye ukurasa wa juu wa gazeti la kila siku la Tanzania liitwalo Mwananchi.
 
Habari hiyo inaeleza kwamba Askofu wa kanisa la Anglikan jimbo la Dar es salaam,Dk Valentino Mokiwa ameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina kwenye taasisi za dini nchini kutokana na mahubiri yanatotolewa na baadhi ya taasisi hizo kuwa kinyume na mapenzi ya Mungu.

Ameongeza kuwa serikali isiishie kusema kwamba wanaogombana wapatane wenyewe ndani,bali sheria za nchi zitumike kila mahali na wasiachwe watu kwa jina la imani mwisho wasiku wakaumizana.

"Serikali imekuwa na wakaguzi wa fedha,basi utaratibu huu uwekwe hadi katika taasisi za kiimani.Serikali inaandikisha zaidi kuliko kukagua hivyo nawakumbusha"

" Siku hizi taasisi za dini ndizo zinazoongoza kwa uvunjifu wa amani,kuchocheana na kufanya vurugu ndani na mapinduzi,pia kubishana na kufanya mambo yasiyoendana na taasisi hizo" alisema Mokiwa.

Soma hapa chini habari hiyo kamili kama ilivyoandikwa na gazeti la Mwananchi.
 
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment