USIKOSE SEMINA HII KUBWA YA UJASILIAMALI JIJINI MWANZA KUTOKA KWA VVM.



Ile kampuni bingwa ya masuala ya ujasiliamali kanda ya ziwa VVM yaani Vitu Vitatu Muhimu kampuni inayoongozwa na mwanamama mjasiliamali Coletha Shindika inakuletea mafunzo ya ujasiliamali kwa nadharia na vitendo jijini Mwanza.

Njoo ujifunze kutengeneza barafu aina ya chostik kwa mashine ya kisasa kwa gharama nafuu,jinsi ya kutengeneza faida kutoka Sh 30,000 hadi sh 50,000 kwa siku na kuendelea.

Pia utakutana na wafanyabiashara wa kimataifa kutoka jijini Dar es salaam,Mwanza na nje ya nchi.Mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa siku tatu kwa gharama ya Tsh 10,000/=tu kwa siku zote tatu.

Kubwa zaidi kwa watakaohudhuria mafunzo hayo ni kwamba wataunganishwa katika mfuko wa bima ya afya bure pamoja na mikopo kwaajili ya kuanzisha biashara.

Mafunzo yataanza kuanzia tar 25-27/4/2017 kila siku kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni katika ukumbi wa Buzuruza Plaza jijini Mwanza huku vitabu na vyeti vikitolewa bure kwa wote watakaohudhuria.

Tiketi za ushiriki zinapatikana katika vituo vifuatavyo:Kwaneema fm radio kiloleli,Buzuruga Plaza pamoja na ofisi za Dstv zilizopo mkabala na jengo la PPF Plaza.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba:0765055239/0629516350.Wahi sasa kwani nafasi ni chache.Watu wote mnakaribishwa!

Semina hii imedhaminiwa na Kwaneema fm radio,Bank ya Posta Tanzania pamoja na mfuko wa Pensheni wa PPF.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment