YAMETIMIA!MADAM FLORA KUFANYA BONGE LA HARUSI JIJINI MWANZA,ATAZINDUA ALBUM NA KITABU CHA SIRI ZAKE SIKU HIYO YA HARUSI!



Hayawi Hayawi sasa yamekuwa,lile tukio kubwa kabisa lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi hatimaye siku imewadia.

Si kingine bali ni harusi ya mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania anayefahamika kwa jila la Madam Flora ambaye atafanya sherehe kubwa ya harusi tar 30/4/2017 katika ukumbi wa Kishimba Beach iliyopo mkabala na Rock Beach Garden jijini Mwanza nchini Tanzania kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.

Madam Flora anawakaribisha watu wote kwenye sherehe hiyo ya aina yake ambapo siku hiyo itaambatana na uzinduzi wa album yake mpya kabisa inayokwenda kwa jina la 'WAKATI WAKE' lakini pia kitabu kipya kinachoitwa 'SIRI ZA FLORA MBASHA' kitazinduliwa katika sherehe hiyo.

Kadi za harusi hiyo zinapatikana kwa Tsh.50,000/=Single na Tsh.70,000/=-Double.Kadi zinapatikana kwenye hotel ya Belmont Fair Mount Hotel zamani JB Belmont Hotel,wahi sasa kadi yako maana kadi ni chache na hazitauzwa mlangoni siku ya sherehe.

Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania watakuwepo ambapo Madam Flora ataimba nyimbo zake zote kali Live katika sherehe hiyo.

Vazi la sherehe hiyo ni rangi nyeupe hivyo basi unaombwa kuja ukiwa umevalia rangi nyeupe.Kwa Mawasiliano Zaidi piga simu namba 0758105014/0655105014.Watu wote mnakaribishwa!
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment