HONDWA MATHIASI KUSAIDIA YATIMA NA WAJANE KUPITIA UZINDUZI WA ALBUM YAKE YA NANI KAMA MAMA

Ni tamasha kubwa kabisa la uzinduzi wa Album yake mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza anayeitwa Hondwa Mathiasi Album hiyo inatwa NANI KAMA MAMA.

Uzinduzi huo utafanyika jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba tar 20.11.2016 siku ya Jumapili kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 Jioni.Uzinduzi huo hautakuwa burudani tu bali unaenda mbali zaidi kwani sehemu ya mapato yatakayopatikana yatasaidia watoto yatima na akina mama wajane.

Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili pamoja na kwaya kutoka maeneo mbalimbali chini Tanzania na nje ya Tanzania watakuwepo kama vile:Bahati Bukuku,Ambwene Mwasongwe,Christopher Mwahangila,Emmanuel Mbasha,Betty Lucus,J.Samson(kutoka Marekani),Kihayile Group,Manonga Clasic,Emmanuel Mwasasumbwe,Vanesa Laban,Emmanuel Mwakisepe,Ngwena na wengine wengi watakuwepo.Orodha itaongezeka.
 

































Mshehereshaji yaani MC katika hafla hiyo atakuwa Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji.Kiingilio ni Tsh.3,000 kwa watu wazima na Tsh.1,000 kwa watoto.

Usipitwe na uzinduzi huu ambao hakika utakuwa wa aina yake,kwani Hondwa Mathiasi amepania kufanya suprise kubwa kwa jiji la Mwanza na viunga vyake.

Hondwa Mathiasi ametamba sana na nyimbo kama vile Mwanaume,Uinuliwe,na sasa wimbo wa Nani kama mama ambao ndio umebeba album inayozinduliwa siku hiyo.

-Tazama wimbo wake Hondwa unaoitwa Uinuliwe


-Download/sikiliza wimbo wa Hondwa unaoitwa Nani kama mama
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment