ANZA MWAKA 2017 KWA HAFLA HII KUTOKA KANISA LA HOLY GOST REVIVAL MINISTRY


Askofu Mkuu Wa Kanisa La Holy Ghost Revival Ministry Bishop Josephat Magumba Akishirikiana Na Kamati Ya Maandalizi Wanakuletea Kongamano la maombezi na kusifu linalofahamika kama Family day.

Hii itaanyika jumapili ya tar 1/1/2017 kwenye kanisa la Holy Ghost Revival Ministry lililopo igoma miti ya Nyerere.

Akizungumza na Promover.com katibu wa kanisa hilo Happiness Steven amesema kuwa mbali na maombi na maombezi na kusifu pia kutakuwa na chakula cha pamoja na yatima na wajane ambao wataalikwa katika hala hiyo.

Aidha Bi Happines ametoa wito wa wakazi wote wa Mwanza kujitokeza kwa wingi siku hiyo wakiwa na chochote kwaajili ya yatima na wajane kama vile nguo,chakula,pesa na zawadi mbalimbali kama inavyoelekezwa na neno la Mungu katika Yakobo 1:27.


Waimbaji mbalimbali watakuwepo katika hafla hiyo pamoja na ugeni maalumu kutoka kwa viongozi wa Promover Manegement.Watu wote mnakaribishwa ni bure kabisa hakuna kiingilio.Kwa Mawasiliano Zaidi Piga Simu Namba: +255757961279/+255763354754/+255767818189.
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment