VIDEO ALBUM YAKE MANONGA CLASSIC-SINA HOFU KUINGIA MTAANI HIVI KARIBUNI

 

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za njili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Manonga Classic anatarajia kuachia album yake mpya ya video inayofahamika kwa jila la 'SINA HOFU'.

Manonga Classic ameidokeza Promover.com kuwa album hiyo yenye video za viwango vya kimataifa itakuwa mtaani hivi karibuni ikwa imesheheni nyimbo mbalimbali kama vile Sina Hofu,Usishindane,Rudi,Acha nikuimbie na nyingine nyingi.

Manonga amesema album hiyo ameitengeneza katika mazingira(location)mbalimbali nchini Tanzania huku pia ikiwa imesheheni waimbaji mbalimbali mahili wa nyimbo za njili kutoka ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine Manonga Classic amewaalika wasambazaji ambao wangependa kusambaza album hiyo ndani na nje ya nchi kuwasiliana na Meneja wake kupitia simu namba:0752690120 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment