Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesema suala
la kutooa kwa mapadri ni “zawadi kwa Kanisa” na si hiari, akiondoa matumaini
kwa viongozi hao wa kidini kuoa.
"Binafsi nadhani suala la ukapera ni zawadi kwa Kanisa," Papa
aliwaambia waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 28) wakati akiwa kwenye
ndege akirejea Vatican kutoka Panama alikohudhuria Siku ya Vijana Duniani.
"Pili, sidhani kama suala la hiari katika ukapera linatakiwa
liruhusiwe. Hapana," alisema.
Papa hata hivyo alikiri kuwa “kuna uwezekano kwa sehemu zilizo mbali
kufikika ", kama visiwa vya Pasific au Amazon ambako alisema "kuna
umuhimu wa huduma za kipadri ".
"Hili ni suala linalojadiliwa na wanathiolojia, si uamuzi
wangu," alisema.
Papa huyo raia wa Argentin amekuwa akisema kila mara kuwa
hakuna zuio la kudumu kwa watu waliooa kuwa mapadri na hivyo suala hilo
linaweza kubadilishwa.
Saint Peter (Mtakatifu Petro), kanisa la kwanza la papa,
lilikuwa na mama mkwe, kwa mujibu wa Biblia.
Ukapera uliingizwa karne ya kumi na moja, inawezekana baadhi
ya sababu zilikuwa ni kuzuia uzao wa mapadri kurithi mali za kanisa.
Baadhi, ndani ya Kanisa, wanaamini wakati umefika wa
kuungana na makanisa mengi ya Katoliki ya mashariki kuruhusu wanaume waliooa
kuvaa majoho ya upadri. Mapadri walioa wa Kanisa la Anglikana ambao wanataka
kujiunga na Kanisa Katoliki, wameshakaribishwa.
Kiongozi wa pili kwa mamlaka wa Vatican, Kardinali Pietro
Parolin, aliwahi kusema katika mahojiano mwaka jana kuwa kanisa “kidogokidogo
litaangalia suala hilo kwa mapana" lakini akasema hakutakuwa na mabadiliko
ya haraka.
Source:AFP
0 maoni:
Post a Comment