MTOTO WA ROSE MUHANDO,ESSAU AMANI NDIYE MWIMBAJI ANAYEFATILIWA SANA NA MAMIA YA WATU MTANDAONI,APEWA TUZO NCHINI KENYA

 

Kuna usemi usemao 'Mtoto wa nyoka ni nyoka' na ule mwingine usemao 'Maji hufuata mkondo'.Msemo huo umeonekana kutimizwa na Annoint Essau Amani,mtoto wa Malkia wa mziki wa injili nchini Tanzania mwanamama Rose Muhando,baada ya kijana huyo kutwaa tuzo ya Afrika Mashariki na kati.

Annoint Essau Amani kwa sasa ndiye mwimbaji bora wa kiume katika ukanda wa afrika mashariki na kati,baada ya kutwaa tuzo iliyotokana na wimbo wake wa 'SuperStar' baada ya kuongoza kwa kufuatiliwa sana licha ya wimbo huo kuwa na muda mfupi tangu kuachiwa mwezi septemba mwaka huu,katika album yake ya kwanza inayoitwa 'Vuruga'.
 
Tuzo hiyo ilitolewa tarehe 2/10 mwaka huu katika hafla maalumu iliyofanyika ukumbi wa Nairobi Cinema huko nchini Kenya. 

 
Akizungumza na PROMOVER.COM Amani anasema hadi anapewa tuzo wimbo huo wa SuperStar ulikuwa umefuatiliwa na mashabiki wapatao 425,000 hivyo kuongoza kama wimbo uliofanya vizuri mitandaoni kwa mwaka 2016.

Waandaaji wa Tuzo hiyo ni kituo cha redio cha Biblia Husema,kupitia kipindi cha Mavuno kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu nchini Kenya anayeitwa Mwanambui,ambapo hivi karibuni kipindi hicho kilitwaa tuzo ya kipindi bora kwa mwaka 2016 nchini humo.

Amani anasema hakuwahi kufikilia kufikia mafanikio makubwa kama hayo aliyofikia kwani yeye ni mwimbaji mchanga tu ambaye asingeweza kushindana na wakongwe bali ni kwa wema wake Mungu.

"Namshukuru sana Mungu pamoja na mashabiki wangu kwa kuniwezesha katika hili,naamini hii inatokana na maono ambayo nimeyapata mwaka juzi ndotoni,ambapo Yesu alinitokea na kuniambia nikikubali kupokea wimbo huo(SuperStar)na kuufikisha,atanivusha mara saba ya alipo Rose Muhando".Alisema Amani 

-Tazama hapa Amani akieleza hisia zake baada ya kupokea Tuzo hiyo:
 


-Kuhusu maono ya kutengeneza wimbo wa SuperStar aliyoyapata akiwa ndotoni,Tazama hapa chini akielezea zaidi:
  

-Wimbo wa SuperStar,uliompa tuzo Amani ndio huu hapa chini,utazame sasa:
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment