Miaka michache baada ya kuzinduliwa kwa hekalu moja
la dini mseto kule Ujerumani linalojulikana kama CHRISLAM,likikusanya dini zote
chini ya paa moja,dunia imestaajabu tukio lingine muhimu kuelekea kutimia kwa
unabii wa Yohana(Ufunuo 13),baada ya wasomi wawili kuchapicha kitabu kimoja
kinachojumuisha vitabu 66 vinavyounda Biblia na aya zote zinazounda Quran
ili kuchukua nafasi ya Biblia na Quran zinazotumika kwa sasa.
Wasomi hao Safi Kaskas na Dk.David Hungerford
waliobobea katika tafsiri ya Quran na Biblia,wanadai kuwa kitabu hicho kinachokusanya
kwa pamoja maudhui ya Biblia na yale ya Quran,kitakuwa daraja muhimu kufikia
umoja wa kidini,utakaowafanya wanadamu kumwelewa Mungu vyema na hivyo kusali
pamoja bila kusigana kama ilivyo sasa.
Wawili hawa pia wanatajwa kuwa ni werevu katika
kutafsiri vitabu vya dini za Kiislamu na Kikristo,kwa kujibu maswali magumu yanayohusu
misimamo ya imani na pia ni wajumbe katika baraza la Kufikia Umoja wa Kidini
liitwalo Bridges to Common Ground.
Kulingana na taarifa ya mtandao wa Christian Post,wasomi hao wawili wanatimiza unabii kwa
kulainisha misingi yenye kukinzana baina ya Uislamu na Ukristo na kuweka njia
sawa kufikia hatma ya dunia hii ya kuwa chini ya mtawala mmoja, dini moja na
serikali moja ya dunia na kwamba jukumu walilopewa wametimiza kwa mafanikio
makubwa.
Nani amewatuma kufanya kazi hiyo na wanafanya kwa maslahi ya nani?Hayo ni maswali yaliyoibuliwa na wasomi wapinzani baada tu ya kutolewa hadharani kwa kitabu kipya mbadala wa Qurani na Biblia zinazotumika kwa sasa.
Inaelezwa kuwa kitabu hiki kinaandaliwa kama
mwongozo wa ukamilishwaji wa kazi ya ChriSlam,ili kuipitisha kwa siri katika
mabaraza ya makanisa na kupata msimamo mmoja kabla ya kukabidhiwa Umoja wa Mataifa
katika kile kinachoonekana kuwa ni kujenga umoja wa kweli wa kidini na
kufutilia mbali vitabu vyenye tafsiri inayounga mkono ugaidi.
Chanzo:Gazeti la Nyakati
0 maoni:
Post a Comment