Bunge la Norway limepitisha rasmi sheria inayoruhusu
watoto wenye umri wa miaka sita na kuendelea kubadili jinsia zao na kuifanya
kuwa nchi ya tano duniani kuruhusu sheria hiyo.
Kupitishwa kwa sheria hiyo kunatoa
kibali kwa raia wa taifa hilo kubadili maungo tangu wakiwa watoto wenye umri wa
miaka sita kwa kutakiwa kujaza fomu maalumu kupitia mtandao bila kufanyiwa
oparesheni wala ushauri wa daktari.
sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Norway juni
mwaka huu inaifanya nchi hiyo kuwa ya tano duniani kuwaruhusu watoto kubadili
jinsia zao baada ya Malta.
Aidha wakati wazazi nchini malta wakitaka uthibitisho wa kimahakama kuhusu uhalali wa suala hilo nchini Norway watoto wanashughulikia wenyewe wakitumia utaratibu huo huo kama watu wazima.
Inadaiwa kuwa wapiga kampeni wa masuala ya kubadili
jinsia nchini humo wameungana mkono sheria hiyo mpya huku wataalamu wakitoa
angalizo dhidi ya kuungwa mkono huko kwamba kutaleta madhara makubwa kwa watoto hao watakapokuwa
watu wazima.
Sheria hiyo itamtaka mtu yeyote anayetaka kubainisha jinsia anayotaka
ambayo haifanani na ile aliyoumbiwa na
mungu,kujaza fomu hiyo kupitia mtandao na kuirejesha huku akiwa ameweka wazi
maamuzi yake.
ikiwa mhusika amekamilisha mchakato
mzima wa kutaka kubadili jinsia au maungo yake itamlazimu kupata namba ya
kitambulisho kipya cha uraia itakayomruhusu kufanya marekebisho katika hati
yake ya kusafiria,lesseni ya gari,cheti
cha kuzaliwa kadi za benki na fomu nyingingine za utambulisho.
Inadaiwa kuwa hadi sasa zaidi ya raia wa norway 250
wameshapeleka maombi yao kwa ajili ya kubadili maungo yao na kisha kubarikiwa
na serikali ya nchi hiyo.
"Nimekutana na vijana kadha wa kadha ambapo wananiambia
kwamba sheria hiyo imefanywa kuwa nyepesi zaidi
wengine wamejiondoa kutoka kwenye
eneo hili la gaza" alisema wazri wa afya nchini humo Benti Hoie
Aliongeza kuwa watunga sheria walililfikia hilo
kwamba linahitaji kiasi fulani cha muda kati ya maombi na sheria hii ya
mabadaliko ili kuangalia matokeo lakini
walilitupilia mbali wazo hilo.
Sheria hiyo inamtaka mtu ayetaka kubadili jinsia
zake kwanza kupatiwa matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kubadili homoni
zake na jaribio la kufanyiwa upasuaji wa jinsia kabla ya kuruhusiwa rasmi kubadli maungo yake.
Kwa mujibu wa taarifa zaidi kutoka nchini humo taasisi inayohusika na masuala ya jinsia ya Norwegian Association For Gender And Sexual Diversity,ndiyo iliyopunguza umri wa nchi hiyo kufanyiwa upasuaji wa kubadili maungo yao kutokana na miaka saba hadi sita ya sasa.
Taasisi hiyo inadai kuwa watototo wanatakiwa kuanza
na mabadiliko hayo ya kubadili jinsia zao wakiwa bado kwenye ngazi ya madarasa
ya chini na siyo ya kati.
Baadhi ya raia nchini humo wanasema Raia yeyote
nchini humo anaweza kufanya maamzi ya kugeuza maungo yake ya uzazi na siyo
kuangalia umri.
Raisi wa kituo cha benjamini kinachohusika na masuala
ya jinsia na kutoa matibabu kwa wale wanaofanyiwa upasuaji wa kubadili maungo
yao Mikael Scott aliendelea kupigilia msumari sheria hiyo kwa kutaka
baadhi ya mambo kufanyiwa kazi kwanza.
Alisema ni imani yake kwamba Norway itafuata
taaratibu za utoaji ushauri kwa watu wanaotaka kubadili jinsia zao.
Makundi mengine yaliyoonyesha kupinga hatua iliyofanywa na bunge la nchi hiyo kupitisha
sheria ya kuruhusu raia wake kubadili jinsia zao kinyume cha mapenzi ya mungu,yaliitaka serikali ya nchi hiyo kufikiria upya.
"Tuna wasiwasi kuhusu uelewa wa wanasayansi kuhusu
hili inamaanisha nini kwa watoto kupandikizwa jinsia zingine!kuna upungufu wa utafiti zaidi
kuhusu hili kwa nguvu zote tunahisi kuwapo kwa tahadhari juu ya hili".Ni matamko
ya baadhi ya makundi ya watu nchini humo wakionesha kutounga mkono hatu hiyo.
0 maoni:
Post a Comment