SEHEMU YA 4 YA USHUHUDA WAKE MANONGA CLASSIC | MKASA WA MAMA WA KAMBO

Karibu tuendelee na sehemu ya nne ya ushuhuda wa kweli wa mwimbaji Manonga classic.Ushuhuda unaitwa 'Mkasa wa Mama wa Kambo'.



AWALI YA YOTE NIWAOMBE RADHI SANA KWA WALE NILIOWAUMIZA MIOYO YENU SIKUJUA KAMA ITAWAGUSA HII KITU HIVYO NAOMBA MNIWE RADHI NIIMALIZIE HII KITU.

BAADA YA KUWA NIMEPOTEZA FAHAMU KWA KILE NILICHOKIONA WAKATI WA USIKU ULE NDIPO WENZANGU WALIPONIPITIA MAJIRA YA SAA KUMI KUELEKEA ALFAJILI WAKANIKUTA NIKIWA NIMEZIMA KABISA NA NDIPO WALIPOANZA KUNIAMSHA BAADA YA MUDA NIKAWA NIMEZINDUKA WALIPONIULIZA MBONA KAMA KUNA TATIZO LIMETOKEA NAMI SIKUWAELEZA CHOCHOTE NILIRUDI NYUMBANI NIKIWA NA MASWALI MENGI MAMA YANGU ALINIPA POLE NDIO UNAEMUONA HAPO KWA PICHA.

NILIACHA KAZI YA UVUVI WA USIKU NA KUANZA KUFANYA KAZI YA UVUVI WA HASUBUI SAA MOJA HADI SAA NNE ASUBUI NILIENDELEA VYEMA NA KAZI HIYO SIKU MOJA NIKIWA NIMEAMKA ASUBUHI NA KUKUSANYA VIFAA VYANGU VYA KAZI NIKACHUKUA MTUMBWI NA KUELEKEA ZIWANI.NILIPOFIKA PEMBEZONI MWA ZIWA NILIUFUNGA MTUMBWI WANGU KWA KAMBA KWENYE MTI ILI UWE KATIKA HALI YA UTULIVU NIENDELEE KUVUA.

WAKATI NIKIWA NAENDELEA KUVUA KUMBE MAMBA MKUBWA ALIKUWA ENEO LILE NAMI PASIPOKUWA NA HABARI NILIENDELEA KUVUA
GHAFLA NAFSI YANGU IKAJAWA NA HOFU NA WASIWASI MKUBWA NIKAWA KAMA NASIKIA SAUTI PEMBENI YANGU IKINIAMBIA ONDOKA ENEO HILI SIKUJUA NIKWANINI KILA HATARI ILIPOKUWA IKINIKARIBIA NAKUWA KAMA NASEMESHWA NA MTU NISIE MUONA.NILIPOANZA KUFUNGUA KAMBA YA MTUMBWI NA KUANZA KUPIGA KASIA KUTOKA ENEO LA TUKIO GHAFLA NILISIKIA KISHINDO KIKUBWA SANA KUMBE YULE MAMBA ALIKUWA AMETEGA CHINI YA MTUMBWI WANGU ALITANDIKA MKIA WAKE KATIKA MTUMBWI WANGU ILI MTUMBWI WANGU UYUMBE NIWEZE KUINGIA MAJINI NAMSHUKURU MUNGU NILIPATA UJASIRI WA KUUBARANSI MTUMBWI WANGU GHAFLA UPEPO ULITOKEA NA KUNISAIDIA KUUPUSHI MTUMBWI WANGU NA KUFANIKIWA KUTOKA KATIKA MAJI.


NILIAMUA KUACHANA NA KAZI ILE YA UVUVI NA KUFANYA KAZI ZINGINE ZA HAPA NA PALE ILI MAISHA YAENDELEE MBELE.

SIKU ZIKAENDA MIAKA IKAENDA MAISHA YAKAWA BADO NISHIDA NA TAABU NYINGI MUDA MREFU NIKAWA NIMEPOTEZANA NA YULE MAMA WA KAMBO NA MAWAZO YAKE YOTE AKAWA ANAJUA TULISHAKUWA MACHOKOLAA WATOTO WA MITAANI NA NDIVYO AKAWA ANAWASIMULIA RAFIKI ZAKE NA NDUGU ZAKE KUWA TULISHAKUWA WAMITAANI.


PALE NYUMBANI KWA MAMA MZAZI ALITOKEA DADA MMOJA ALIYENITAFUTIA KAZI KWENYE KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA STATIONARY.

NAMSHUKURU MUNGU NILIZUNGUKA NA ILE KAMPUNI TAKRIBANI MIKOA YOTE YA TANZANIA UTENDAJI WANGU WA KAZI ULIKUWA NIMZURI NA BOSI ULIMVUTIA HATA KUFIKIA KUTOLEA MFANO KWA WAFANYA KAZI WENZANGU KUMBE KITENDO KILE KILIWACHUKIZA SANA WENZANGU NA KUANZA KUWA WANANIFANYIA VISA VINGI ILI BOSI ANICHUKIE.


WALIANZA KUFICHA VITU NA KUSEMA NIMEIBA WALIANZA KUHARIBU VITU NA KUSEMA NI MIMI NDIPO BOSI ALIPOCHUKIA NA KUANZA KUNIPUNGUZIA MSHAHARA WANGU KAMA ILIKUWA NALIPWA ELFU KUMI KWA SIKU BASI NALIPWA ELFU TANO.

HALI HIYO ILIZIDI NAKUFIKIA HATUA YA KUNIKATISHA TAMAA YA KUENDELEA NA KAZI ILE.


NDIPO NILIPOAMUA KUACHANA NA ILE KAMPUNI NA KURUDI NYUMBANI KUANGALIA USAWA MWINGINE.BAADA YA KURUDI NYUMBANI SIKU MOJA NILIJISIKIA NIENDE NIKAMSALIMIE YULE MAMA WA KAMBO NIKIDHANI PENGINE LABDA ALISHAKUWA MTU MWEMA KUMBE NILIVYOTARAJIA VILE HAIKUWA VILE SIKU YA KWANZA NILIENDA KUMUONA NA AKAWA KAMA AMEPIGWA BUTWAA KUNIONA MAANA HAKUTARAJIA KAMA ANGEKUJA KUNIONA TENA.NILIMSALIMIA NA AKANIITIKIA KINYONGE SANA NIKAMA HAKUFURAHISHWA NA UWEPO WANGU MACHONI PAKE.

SIKU YA KWANZA ILIPITA KUMBE SIKUJUA YULE MAMA KAMA ALIKUWA AMENIANDALIA MTEGO WA KUNIPOTEZA KABISA.

SIKU ILIYOFUATA NIKIWA NIMEENDA KUMSALIMIA RAFIKI YANGU PALE JIRANI NA NYUMBANI ANAPOISHI YULE MAMA WA KAMBO NIKIWA NIMETULIA NDANI NAENDELEA NA MAZUNGUMZO NA RAFIKI YANGU NDIPO MLANGONI IKASIKIKA IKIPIGWA HODI KUMBE NIMAASKARI WAMETUMWA KUJA KUNIKAMATA KWA MARA YA KWANZA NAINGIA KWENYE MIKONO YA POLISI PASIPOKUJUA KOSA LANGU NI NINI WALINICHUKUA NILIPOTAKA KUWAULIZA WALINIAMBIA KUWA KUNA MAMA NILIMIPIGA NIKAWA NIMEMUUMIZA VIBAYA HIVYO NINAITWA NIKATOE MAELEZO KITUONI.

NILIPOFIKA KITUONI NILISHANGAA KUMUONA YULE MAMA WA KAMBO AKIWA KITUONI NA SURA YAKE IKIONEKANA KAMA YA MTU MWENYE GADHABU SANA NILIPOFIKA WAKANIULIZA UNAMFAHAMU HUYU NIKAJIBU NDIO NAMFAHAMU ALIKUWA MKE WA BABA YANGU.

WAKASEMA AMEKUSHITAKI KWA KOSA LA KUMTISHIA KUMUUA MIMI NILIKATAA NDIPO ALIPOULIZWA YEYE KWAMBA UNAMSHITAKI AMA UNAMUONYA YEYE KWA HARAKA KABISA AKASEMA NINAMSHITAKI PALE PALE NIKAVULIWA VIATU NA MKANDA NA VITU VYANGU VINGINE NILIVYOKUWA NAVYO KABLA SIJATUPWA SERO NILIOMBA RUHUSA YA KUTOA TAARIFA KWA NDUGU ZANGU KUWA NIMEKAMATWA NA NIKO KITUO CHA POLISI NA BAADA YA KUMALIZA KUTOA TAARIFA NDIPO NILIPOTUPWA SERO HAPO NDIPO NILIPOIONA DUNIA CHUNGU NA NZITO NA MAISHA YA MISUKOSUKO YAKAANZA UPYA FURAHA YA YULE MAMA IKATAWALA NA KUONA SASA AMENIKOMESHA...

...HISTORIA YA MAISHA YANGU NITAKUJA KUIHITIMISHA KWENYE SEHEMU YA TANO NA NDIPO UTAJUA NILIISHIA WAPI BAADA YA KUTUPWA SERO. 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment