ULE MKESHA WA MAOMBI NA KUFUNGULIWA UMEREJEA TENA,KAA TAYARI


Huduma ya Devine Inspiration For All,chini yake mtu wa Mungu Frighton Semeon,imekuwa baraka sana kwa watu mbalimbali kote nchini ambapo kwa siku za hivi karibuni huduma hiyo imeendelea kuwabariki wakazi wa kanda ya ziwa.

Jiji la Mwanza limekuwa kati ya maeneo ambayo huduma hiyo imeendelea kuwabariki wakazi wake ambapo kwa upendeleo mkubwa Mtu wa Mungu Frighton Semeon anaileta tena huduma hiyo siku ya ijumaa ya tarehe 21/10/2016.Ni kuanzia saa mbili usiku hadi asubuhi katika Hotel ya GoldCreast.

Je!huduma hii inahusu nini hasa!

Ni Huduma ya maombi na kufunguliwa ambapo mkesha maalumu wa maombi huanyika.Katika mkesha huo mtumishi wa Mungu Frighton ambaye Mungu anamtumia katika kuwatambua watu na maisha yao,humuona mtu mmoja mmoja na maisha yake yote,anakotoka alichofanya au kufanyiwa huku akiwapa mwongozo wa kiroho jinsi ya kutatua matatizo yanayomkabili.

Ili kudhihirisha nguvu ya Mungu,watu mbalimbali wanaohudhulia mikesha hiyo huwa wakielezwa matatizo yao na jinsi ya kuyatatua kupitia maombi.

Baadhi ya watu waliowahi kuhudhulia mkesha huo wakizungumza na PROMOVER.COM wanasema wamepokea mambo makubwa sana ambayo hawakuwahi kuyafahamu maishani mwao ikiwa ni sambamba na jinsi ya kuyatatua,baraka nyingi na uwezo wa kusimama imara kiimani.

Kama upo kanda ya ziwa hasa Mwanza au hata nje ya kanda ya ziwa,fanya uwezavyo siku ya ijumaa kuanzia saa mbili usiku wa tarehe 21/10/2016 usipitwe na mkesha huo.Njoo upokee baraka zako,Njoo ufunguliwe njoo ufahamu uhusiano wa matatizo yako na kushindwa kufanikiwa maishani,njoo uwekwe huru kutoka vifungo vya shetani.Mwenyezi mungu akubariki sana. 
 Kumbuka Hakuna kiingilio,ni bure kabisa Wote mnakaribishwa!
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment